vendredi 4 juillet 2014

MAISHA YA PADRI SYAMINYA NGOLOMA Roger, aa.


Ndugu yetu Padri SYAMINYA NGOLOMA Roger, wa shirika la waasomptionnite. Alizaliwa MUNGO (Masereka) diocèse ya Butembo-Beni tarehe 13/07/1969, Baba KAMATE Denis na mama KAVUGHO Astrida. Alibatizwa 22/09/1969 pa parokia Masereka. Alisomea pa shule ya msingi Itundula mpaka 1982, Institut Kitsimba (1982-1989) na Institut Malkia wa Mbingu (1989-1991). Aliwasiliana na mapadri waassomptionniste kupitia mikutano ya vijana wa uito pa Kambali.
    Baada ya kumaliza mtihani wa kimataifa aliendelea kufikiria uito wake akianza masono ya uchumi na biashara kwa ISGA Butembo (1991-1992). Alikubaliwa kwa postulat 1992-1993 pa Kitatumba. Alikubaliwa kwa noviciat Lwanga 1993-1994 chini ya uongozi wa Padri Lucas Chuffart. Alifanya naziri za lwanza hapa Kitatumba 28/08/2014. Alienadelea na utawa wake akisoma philosophia pa Bulengera 1994-1997. Mwaka 1997-1999 waongozi wa shirika walimuruhusu kuendelea na masomo aliyoanza kabla kuingia katika utawa. Mwaka 1999 alifanya naziri za milele hapa 31/07/1999. Kwa miaka miwili alifanya kazi katika shuruli za uchumi wa jimbo pa Kambali pamoja na padri David Milonde (1999-2001). Kwa miaka 2001-2004 alitumwa Nairobi kwa masomo ya teologia pa Hekima College. Alimalizia masomo hayo pa Kinshasa mwaka 2005.
Kutoka Kinshasa alitumwa Kasando kama muweka hazina ya jumuiya. Alipewa daraja ya ushemasi 09/11/2006 na Askofu Sikuli Melkisedeki pa Cathedral. Alipewa daraja ya upadri pa Kitatumba tarehe 24/11/2008 na Mgr Mariano Crochiata, Askofu wa Noto, aliyefika kwa ziara ya upacha hapa Butembo.
Baada ya upadrisho aliendelea kuwa padri msaidizi pa Kasando. Mwaka 2010 alitumwa Oicha. Mwaka 2013 alitumwa Kinshasa kwa mradi wa ukulima huko Bateke. Alizoea kupanga huko zaidi ya juma mbili akilima na tingatinga tuliyopewa na serikali, wizara ya ukulima.
    Tangu miaka iliyopita tulijua alikuwa na shida ya afia sababu ya ugonjwa wa moyo. Kila mara alipokuwa na ugonjwa mwingine, shida ya moyo ilikuwa inajitokeza pia na kutatiza zaidi matibabu. Juma iliyopita alilazwa kwa kituo cha afia cha Mabikira Oblates wa Masina. Siku ya kwanza alipelekwa Clinique Bondeko. Mpaka jioni tuliwasiliana kwa simu yake akiongea yeye mwenyewe. Hatukujua kwamba kuna hatari yoyote. Asubui ya siku ya pili alikufa kwa shida ya moyo na ya figo.
    Tunamjua Roger kama mtawa na padri aliyependa Shirika kama jamaa yake. Alitumika sana kwa uchumi na maendeleo ya miradi ya kujitegemea ya jimbo la Afrika. Japo alikuwa mwana wa pekee wa mama yake, lakini alipokea kila mtu na kupokelewa katika jumuiya yoyote bila ubaguzi wowote. Alikuwa na nguvu na juhudi kwa kazi yoyote aliyotumwa kutimiza. Alijionyesha mtu wa lazima sana katika maandalizi yoyote, shuruli nyingi na sherehe kubwa za kanisa. Alikuwa na marafiki zaidi ya wajamaa wake. Anajuliwa sana kwa visa vingi vya kuchekesha, aliongea sana matukio ya maisha yake mwenyewe na juu ya wengine. Alikumbusha mara nyingi hadisi za zamani katika jumuiya alimokaa. Alipangwa majina mengi sababu ya michezo mingi na maneno ya kufurahisha. Kazi yake ya mwisho ni ya kuendelesha miradi ya ukulima kwa maendeleo ya shirika pa Kinshasa.
Tunamushukuru sana kwa kazi aliyofanya na mfano aliyoonyesha kwa wengine wote wanaohusika katika kazi hiyo. Tunaomba Mungu amuonyeshe rehema yake na ampumzishe kwa amani karibu naye.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire